Ee Baba Lyrics — Light Bearers TZ

 STANZA 1

Ee Baba uliye mbinguni
Jina lako litukuzwe
Asante kwa uzima na afya
Mibaraka yako naiona
Naimba kwa furaha tele
Amani yako imejaa moyoni
Familia yangu yakusifu
Ewe Mungu uhimidiwe
Daima twaziimba sifa zako
Halleluyah usifiwe


Ee Baba by Light Bearers TZ

CHORUS
Nami nitakuimbia
siku zangu zote
Asante Mwokozi
kwa wema wako kwangu X2

Watch Ee Baba by Light Bearers TZ Lyrics Video Here

STANZA 2
Umenipa na mavazi
makaazi nayo kazi pia
nacho chakula mezani kwangu
utukufu wako umejaa tele
sina cha kukulipa Mungu
najitoa kwako maana U kimbilio
maisha yangu nayaleta kwako
Ewe Mungu utawale
Kwani ninayo faida
kuwa ndani yako nawe ndani yangu

Watch Ee Baba by Light Bearers TZ Lyrics Video Here

CHORUS
Nami nitakuimbia
siku zangu zote
Asante Mwokozi
kwa wema wako kwangu X2

STANZA 3
Njooni nyote tumwimbie Bwana
kwa zaburi na vinubi
Mungu aliye mtukufu
astahiliye kutukuzwa
tutangaze neema yake
maana yeye ni mkuu sana
tuimbe na tumshukuru
Mungu wetu atupendaye
atupaye mibaraka kila siku
maishani mwetu

CHORUS
Imbeni wanadamu
pazeni sauti
mwimbieni Bwana
aliye mtukufu X2
Nami nitakuimbia
siku zangu zote
Asante Mwokozi
kwa wema wako kwangu

Post a Comment

0 Comments